LICHA ya kubainisha kwamba wanatambua wapo ugenini mbele ya Simba lakini wameweka wazi kwamba hawatakuwa wanyonge bali watacheza kwa umakini kusaka ushindi leo Uwanja wa Mkapa.
Julien Chevalier,Kocha Mkuu wa ASEC Mimosas alisema kuwa aliwafuatilia Simba katika mechi za ligi ya mabingwa Afrika na kuona uwezo wao.
“Simba ni timu kubwa nimeifuatilia na tumeona kwamba ilikuwa ikifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini licha ya ukubwa walionao tunahitaji ushindi mbele yao.
Hatuna mashaka kwa kuwa maandalizi yapo vizuri na tumefika hapa kwa muda na kuoata saa za kupumzika, imaniyetu ni kuona kazi iliyotuleta inakamilika..
“Tumepata mufa mrefu na sasa tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ambao ninajua utakuwa mgumu ila maandalizi ambaho tumefanya kwa asilimia kubwa yanatupa nafasi ya kushinda ugenini na kupata pointi tatu, ” amesema.
Nahodha wa ASEC Mimosas, Cisse Abdul Karim amesema kuwa licha ya ukubwa wa wapinzani wao hawana mashaka zaidi wanawaheshimu.
Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizi ziliwahi kukutana uwanjani 2003 katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika na ndani ya dakika 180 kila timu.
Simba ilitinga hatua ya mkundi kwa ushi wa jumla ya mabao 4- 2 dhidi ya Red Arrows na ASEC Mimosas ilishinda mbao5-2 dhidi ya Interclube.