DICKSON Job, beki kitasa wa Yanga ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi anatarajiwa kuukosa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.
Job aliibuka ndani ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar ambapo huko pia alikuwa ni nahodha na chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Zuber Katwila ambaye alikuwa anakinoa kikosi hicho kabla ya kuibukia Ihefu.
Hivyo Job atakosa kazi ya kuwazuia washambuliaji wa zamani wa mabosi wake ndani ya mchezo wa ligi.
Sababu kubwa ya Job kuikosa Mtibwa Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari 23,Uwanja wa Manungu, Morogoro ni kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumkanyanga nyota Richardson Ng’ondya wa Mbeya City.
Mchezo wa awali ambao anatarajia kuukosa ni huu wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 15.