UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa mpaka sasa haujapokea barua ya mchezaji wao Bernard Morrison kama ambavyo alielekezwa kufanya hivyo kabla ya kusimamishwa.
Februari 4,2022 Simba ilitoa taarifa rasmi ya kumsimamisha Morrison kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu ya utovu wa nidhamu.
Ofisa Habari wa Simba,Ahmed Ally amesema:”Tulimsimamisha Morrison kutokana na tuhuma za nidhamu ambazo zinamkabili na tukamwambia kwamba anatakiwa kuandika barua kwa mtendaji mkuu wa Simba.
“Hivi ndivyo sheria inatueleza kwamba mtu akituhumiwa basi apate nafasi ya kujieleza ama kuthibitisha kuhusu tuhuma hiyo lakini mpaka sasa hatujapokea baura ya Morrison. Akishatuma barua hiyo sasa manegement, (utawala) itaangalia maelezo yake na itaamua aidha impeleke kamati ya nidhamu ama manegement itaona yenyewe namna ya kulimaliza.
“Kwa sisi tunafahamu kwamba Morrison bado yupo nchini na atakapotoa maelezo tutajua itakuaje kuhusu taarifa za kuodoka ama anakwenda wapi sisi hatujui lakini ambacho tunajua kwamba Bernard Morrison ni kijana wetu bado tunampenda na bado tunamhitaji sana Bernard Morrison tukijiridhisha atarejea kwenye timu,”.