UONGOZI wa Yanga, leo Februari 8,2022 unebainisha kuwa mwendo wa Ligi Kuu Bara katika mechi za ligi umeweka wazi kwamba hauridhishwi na mwendo wa waamuzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Idara ya Habari Yanga,Hassan Bumbuli amesema kuwa mwendo wa waamuzi umekuwa hauridhishi katika baadhi ya mechi.
Bumbuli pia alibainisha kwamba kumekuwa na tofauti kubwa ya muda wa nyongeza kati ya mechi ambazo wao wanacheza pamoja na zile ambazo zinachezwa na Simba.
“Haturidhishwi na mwendo wa waamuzi hivyo tunawaomba wenye mamlaka waweze kulitazama hili ili kuifanya ligi yetu kuwa bora,sisi hatulalamiki ila hii ni tathimini yetu,”.
Kwa upande wa Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa tangu awali aliweka wazi kwamba hawatalalamika kuhusu waamuzi na wenye mamlaka ya mpira bali wanawakumbusha tu.