CHAMA ATUPIA SIMBA IKISHINDA MBELE YA MBEYA KWANZA

CLATOUS Chama,mwamba wa Lusaka ametupia bao pekee la ushindi mbele ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ni bao la kwanza kwa Chama akipachika bao hilo akitokea benchi alipokuwa akisoma mchezo.

Ni dakika ya 85 mpira ulijazwa kimiani na kufanya mashabiki wa Simba kunyanyuka jukwaani.

Unakuwa mchezo wa pili kwa Simba kushinda bao mojamoja Uwanja wa Mkapa baada ya mchezo uliopita kushinda bao 1-0 mbele ya Prisons.

Bao la Chama liliwafanya benchi la ufundi la Mbeya Kwanza kuwafuata waamuzi na kadi ya njano ilitolewa kwa Rolland Msonjo.