UWANJA WA MKAPA MILANGO NI MIGUMU KWELIKWELI, SIMBA 0-0 MBEYA KWANZA

UWANJA wa Mkapa milango ni migumu kwelikweli kwa timu zote mbilo ndani ya dakika 45 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Simba imekwama kuwatungua Mbeya Kwanza ambao nao wamekwama kumtungua Aishi Manula.

Mtu wa kazi chafu Rolland Msonjo anatibua mipango ya Simba inayotengezezwa na Rally Bwalya.

Licha ya washambuliaji wawili kuanza John Bocco na Meddie Kagere kwa Simba bado ngome ya Mbeya Kwanza ipo salama mikononi mwa kipa Hamadi Kadedi.