DELE ALLI NI MALI YA EVERTON, HATALIPWA HATA 1000

DELE Alli amewashukuru Tottenham kwa maisha yake ya soka aliyokuwa akiishi hapo wakati akiitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Kwa sasa Everton imekamilisha usajili wa kiungo Alli kwa usajili huru kutokea Tottenham uhamisho ambao unaweza kufikia pauni milioni 40, (sh. Bilioni 123).

Hata hivyo fungu la kwanza la Alli atapewa pauni milioni 10 akicheza mechi 20 lakini Everton wamebakiza mechi 18 ikimaanisha kuwa kiungo huyo hatapa hata shilingi 100 ya Kitanzania msimu huu.

Raia huyo wa England alikosa namba katika kikosi cha Antonio Conte alifanya vipimo vya afya juzi kabla ya saa chache za dirisha la usajili kufungwa.