BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu za Taifa za Wanawake, Bakari Shime amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio dhidi ya Ethiopia.
Shime yupo na kikosi kazi cha Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite na inatumia Uwanja wa Black Rhino kufanyia mazoezi.
Kwa sasa timu hiyo imeweka kambi Karatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Ethiopia unaotarajiwa kuchezwa Februari 4,2022.