VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kwa sasa wanaipigia hesabu Mbeya City kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa ligi.
Februari 5 Uwanja wa Mkapa Yanga yenye pointi 35 ikiwa nafasi ya kwanza inatarajiwa kumenyana na Mbeya City.
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddien Nabi amesema kuwa ambacho wanahitaji kwenye mchezo huo ni pointi tatu.
“Kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu na ili kupata pointi ni lazima tushinde mchezo wetu.
“Ushindani ni mkubwa na kila timu inafanya kazi kubwa kusaka pointi tatu hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kazi ni kubwa,”.
Kinara wa utupiaji Yanga ni Fiston Mayele mwenye mabao sita na pasi mbili za mabao.