Singida Black Stars Yavunja Benchi Zima la Ufundi Baada ya Kichapo cha TRA United

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kuvunja Benchi zima la Ufundi la timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Othmen Najar kuanzia leo, tarehe 05 Aprili 2026, ikiwa ni muda mfupi baada ya kipigo cha 2-0 dhidi ya TRA United katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Taarifa ya leo Aprili 05, 2026 iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika kipindi cha hivi karibuni.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa klabu hiyo itatoa taarifa kuhusu benchi la ufundi la mpito wakati ikiendelea na maandalizi ya michezo ijayo.