Mshambuliaji nyota wa Mohamed Salah ametangaza rasmi kuwa ataondoka ndani ya klabu ya Liverpool mwishoni mwa msimu huu, akihitimisha safari ya kihistoria ya miaka tisa ndani ya Anfield.
Salah, mwenye umri wa miaka 33, ameondoka akiwa mchezaji huru (free transfer), jambo ambalo limewashtua mashabiki wengi wa soka duniani.
Kupitia video ya kihisia aliyochapisha mtandaoni, Salah alisema:
“Sikuwahi kufikiria jinsi klabu hii, jiji hili na watu wake wangekuwa sehemu kubwa ya maisha yangu. Liverpool si tu klabu ya mpira, ni historia, ni roho.”
Nyota huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea AS Roma na tangu wakati huo amekuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kuichezea klabu hiyo.
Katika kipindi chake, Salah amefunga jumla ya mabao 255 katika mechi 435, rekodi inayomweka miongoni mwa magwiji wa Liverpool.
Kuondoka kwake kunamaanisha kuwa atasalia na mechi chache tu kuongeza idadi ya mabao kabla ya kufunga rasmi ukurasa wake Anfield.