Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo imepata matokeo mabaya katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kusababisha mashabiki wapoteze imani na ule msemo kwamba ‘Kwa Mkapa hatoki Mtu’.
Amesema katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Stade Malien, japokuwa hata wakishinda hawataenda popote, wanataka kuutumia mchezo huo kulinda heshima ya Simba na kurudisha imani kwa mashabiki.