Kuonyesha dhamira yake isiyoyumba ya kuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto za kijamii, kampuni ya Meridianbet imeendeleza msururu wa miradi yake ya kusaidia jamii kwa kugawa vyakula kwa familia zenye uhitaji katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam. Hatua hii inathibitisha kwamba kampuni hiyo haishughuliki tu na michezo ya kubahatisha, bali pia ni nguzo muhimu ya ustawi kwa wananchi wa kawaida.
Tukio hilo limekuwa sehemu ya mkakati mpana wa Corporate Social Responsibility (CSR), unaolenga kuongeza thamani halisi kwenye maisha ya watu. Kupitia msaada huo, familia nyingi zilizokuwa zikikabiliana na upungufu wa chakula zimepokea bidhaa muhimu kama vile unga, mchele, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni, na mahitaji mengine ya msingi, msaada ambao umekuwa faraja ya kweli katika mazingira ya kiuchumi yasiyotabirika.
Akitoa salamu kwa niaba ya kampuni, mwakilishi wa Meridianbet alisisitiza kuwa jukumu lao ni kwenda mbali zaidi ya burudani na michezo. “Tunachokifanya ni zaidi ya jukumu la kampuni, ni wito. Tunatambua kuwa jamii inahitaji mshirika wa kweli anayesimama nao katika nyakati ngumu. Msaada huu ni ishara ya dhamira yetu ya muda mrefu ya kuhakikisha kila familia inapumua, hata kipindi ambacho maisha yamekuwa mazito.”
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Wananchi walionufaika hawakusita kuonyesha shukrani zao, baadhi wakielezea jinsi msaada huo ulivyofika katika kipindi ambacho hawakuwa na uhakika wa mlo wa kesho. Baadhi walisisitiza kuwa msaada wa aina hii unapaswa kuwa mfano unaofuatwa na makampuni mengine nchini, kwani unagusa moja kwa moja maisha ya watu walioko kwenye mstari wa hatari wa umasikini.
Meridianbet, ambayo imejizolea sifa kwa miradi ya kijamii kama vile kusaidia vituo vya watoto yatima, kutoa vifaa vya afya, kuboresha mazingira na kushiriki kampeni za maendeleo ya vijana, inaendelea kuonyesha kuwa mafanikio yake ni chachu ya kutoa kwa jamii. Kampuni imeahidi kuendeleza mikakati endelevu ya kuhakikisha misaada ya kijamii inakuwa sehemu ya utamaduni wake wa kudumu.