Simba SC vs Peto de Luanda, hapa jeuri ilipo kwa wenyeji

Simba SC vs Petro de Luanda ni CAF Champions League hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 23,2025 saa 10:00 jioni.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa jeuri yao ipo kwa mashabiki ambao wamekuwa wakiwapa nguvu katika mechi za ushindani.

“Nguvu yetu mara zote ni mashabiki, mara zote mlipokuja na kujaza Uwanja wa Mkapa huwa tunapata matokeo mazuri. Password ya ushindi wetu ni mashabiki. Mkija kwa wingi uwanjani siku hiyo basi uhakika Mnyama ataondoka na alama tatu.

“Jeuri ya kubaki Uwanja wa Mkapa tunaipata kutoka kwa mashabiki wetu sababu tuna uwezo wa kujaza Uwanja wa Mkapa. Tunabaki hapo sababu ya uwingi mashabiki tulionao, sababu pekee ya sisi kuhama Uwanja wa Mkapa ni labda ufungwe na serikali, natunabaki Uwanja wa Mkapa sababu yenu mashabiki tukijua mnaweza kuujaza, Benjamin Mkapa ni chumba cha baba halali kila mtu na sisi ndio baba wenyewe, baba hakimbii chumba chake.

“Kuhusu Jezi mpya za Ligi ya Mabingwa Afrika zitazinduliwa siku ya Alhamisi Novemba 20, 2025 na baada ya kuzinduliwa zitakuwepo madukani.”