Mbappé Ataka Fidia ya €263m kutoka PSG Amidani ya Mzozo wa Mkataba

Nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappé anadai fidia ya Euro Milioni 263 (takriban TSh 743 Bilioni) kutoka kwa Paris Saint-Germain katika mzozo unaohusu mkataba wake.

Awali PSG ilimshtaki Mbappé, ambaye alihamia Real Madrid mwaka jana, ikidai ilipwe Euro 240 Milioni (takriban TSh 677.3 bilioni), baada ya kukataa uhamisho wa kwenda katika timu ya Al Hilal ya Saudia.

Mbappé (26), awali aliwasilisha malalamiko mwezi Juni kuhusu jinsi alivyotendewa na PSG mwanzoni mwa msimu wa 2023-24.

Anaamini alitengwa na klabu hiyo inayomilikiwa na Tajiri wa Qatar na kufanya mazoezi na Wachezaji ambao klabu hiyo ilikuwa ikijaribu kuwaondoa baada ya kukataa kukubaliana na mkataba mpya.

Ni mazoezi ambayo pia yameathiri Wanasoka wengine na kusababisha muungano wa wachezaji wa Ufaransa kuwasilisha malalamiko yao mwaka jana.