Petro de Luanda wapinzani wa Simba SC CAF Champions League matokeo yao

Petro de Luanda wapinzani wa Simba SC CAF Champions League ni wagumu kwenye mechi zao kutokana na kuwa na ukuta usiopenyeka kirahisi kwa mujibu wa rekodi.

Timu hiyo kwenye mechi 7 za ushindani za hivi karibuni rekodi zinaonyesha kuwa ushindi mechi 5 ikipoteza mechi 2 na hakuna sare matokeo yao ni kushinda ama kupoteza.

Kwenye mechi hizo 7 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 12 huku ukuta wao ukiriuhusu kufungwa mabao manne.

Hawa wanatarajiwa kukutana na Simba SC, Novemba 23,2025 kwenye mchezo wa hatua ya makundi Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.

05/10/2025, Wiliete SC 0-2 Petro de Luanda mchezo wa ligi ya Angola.

18/10/2025, Stade d’Abdjan 0-2 Petro de Luanda, CAF Champions League.

25/10/2025, Petro de Luanda 2-0 Stade d’Abdjan Caf Champions League.
29/10/2025 Sao Salvador 2-1 Petro de Luanda, mchezo wa ligi ya Angola.
01/11/2025, Petro de Luanda 4-1 Libolo, mchezo wa ligi ya Angola.
05/11/2025, Petro de Luanda 1-0 Interclube, mchezo wa ligi ya Angola.
09/11/2025, Petro de Luanda 0- 1 de Agosto, mchezo wa ligi ya Angola.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.