Meridianbet Yaendelea na Moyo wa Ukarimu: Yatoa Msaada Kwa Kituo cha Urekebishaji MRC

Meridianbet wameonyesha tena moyo wa huruma kwa kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa kituo cha MRC Rehabilitation Centre kilichopo Dar es Salaam. Hatua hii imeonyesha jinsi kampuni hiyo inavyoweka mbele ustawi wa jamii kama sehemu muhimu ya utendaji wake wa kila siku.

Msaada huo ulihusisha bidhaa mbalimbali kama vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine za matumizi ya nyumbani, zilizokusudiwa kuboresha hali ya maisha ya watu wanaopokea matibabu kituoni hapo. Kwa Meridianbet, hii ni zaidi ya msaada, ni uwekezaji katika utu, matumaini, na maisha ya wanaopambana kurejesha hali bora ya kiafya na kijamii.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, muwakilishi wa Meridianbet alisema kuwa kampuni hiyo imejenga misingi yake juu ya falsafa ya jamii kwanza. Alibainisha kuwa kila mafanikio ya biashara ni fursa ya kurudisha kwa jamii, hasa kwa makundi yenye uhitaji maalum. “Tunatambua kuwa maendeleo halisi hayapimwi kwa namba pekee, bali kwa namna tunavyogusa maisha ya wengine,” alisema.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Viongozi wa MRC Rehabilitation Centre nao walipongeza hatua hiyo, wakisema msaada huo umefika wakati muafaka ambapo kituo kilihitaji msaada wa vifaa na mahitaji ya msingi. “Meridianbet wameonyesha kwamba kampuni kubwa zinaweza kuwa na moyo wa kusaidia, bila kujali faida bali thamani ya binadamu,” alisema kiongozi wa kituo hicho.

Kupitia miradi yake ya CSR, Meridianbet imeendelea kujijengea nafasi ya kipekee katika kusaidia makundi mbalimbali nchini, ikiwemo watoto yatima, wagonjwa hospitalini, na taasisi za elimu. Kila hatua wanayochukua ni ushahidi wa jinsi kampuni hiyo inavyolenga kuacha alama chanya katika jamii.