Yanga SC kufanya usajili wa mshambuliaji wa kazi

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves inatajwa kwamba wapo sokoni kutafuta mshambuliaji mwingine wa kazi.

Katika eneo la ushambuliaji ni Andy Boyel, Prince Dube hawa wamekuwa wakipata nafasi ya kuanza huku Clement Mzize akiwa nje ya uwanja kutokana na maumivu ya goti.

Licha ya timu hiyo kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika kuwa ni namba moja kwa kufunga mabao mengi ambayo ni 9 baada ya mechi 4 bado hakujawa na kasi katika eneo la ushambuliaji.

Taarifa zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kwenye dirisha dogo mabosi wa Yanga SC wakaongeza mshambuliaji mmoja ambaye atakuja kuongeza nguvu kwenye eneo hilo muhimu.

Mbali na mshambuliaji Yanga SC inasaka kiungo mkabaji eneo la kati kutokana na kutokuwa na mwendelezo mzuri eneo hilo mara baada ya kuachana na Khalid Aucho ambaye kwa sasa yupo kikosi cha Singida Black Stars.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.