Meneja Dimitar Pantev anataka mpira wa kushambulia kwa kasi

MENEJA Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev anataka mpira wa kushambulia kwa kasi ili timu hiyo kupata matokeo mazuri uwanjani.

Kwa msimu wa 2025/26 Simba SC kwenye mechi za nyumbani imekwama kupata matokeo mazuri katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.

Ilikuwa sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Gaborone United na 0-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs. Timu hiyo imekata tiketi kutinga hatua ya makundi na mchezo wa kwanza itaanzia nyumbani.

Novemba 22,2025 Simba SC vs Petro Atletico ya Angola huu mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku ikiwa ni msako wa pointi tatu hatua ya makundi.

Pantev amesema kuwa anapenda kuona wachezaji wakifanya kazi kubwa uwanjani kutafuta matokeo hasa kwa kushambulia na kutumia nafasi ambazo wanazipata uwanjani.

“Kwenye mechi ambazo tunacheza ni muhimu wachezaji kuwa makini na kushambulia kwa kasi lango la wapinzani.Ili kupata matokeo ni lazima kutumia nafasi ambazo unatengeneza hili ni jambo ambalo tunalifanyia kazi eneo la mazoezini,”.

Simba SC mchezo wao uliopita ilikuwa katika Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya JKT Tanzania ilipata ushindi wa mabao 2-1.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.