Wabunge wakimpongeza Dkt. Mwigulu Nchemba baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu kutangaza kuwa Mhe. Rais amemteua kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ujumbe maalum kuhusu uteuzi huo uliwasilishwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri Bungeni leo Novemba 13, 2025.
Uteuzi wa Mbunge huyo wa Iramba Magharibi umewasilishwa Bungeni kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kumthibitisha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.