Steven Mukwala mambo bado Simba SC

Steven Mukwala msimu wa 2025/26 mambo bado magumu kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kukwama kufungua akaunti ya mabao.

Ipo wazi kwamba Mukwala hajawa katika ubora ambao unahitajika kutokana na kukosa nafasi za kufunga anapopata nafasi kwenye mechi za ushindani.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Novemba 8,2025 alikosa nafasi tatu, moja ilikuwa ni clear chance akatoa pasi kwa mlinda mlango wa JKT Tanzania ambaye aliokoa hatari hiyo.

Ni dakika 60 alitumia kwenye mchezo huo alimpisha Jonathan Sowah ambaye alifunga bao la ushindi akitumia pasi ya Morice Abraham kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Kwenye msimamo Simba SC ipo nafasi ya pili baada ya mechi 3, safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 8 ikiwa imekusanya pointi 9 kibindoni.

Mukwala amecheza jumla ya mechi mbili akikosekana katika mchezo mmoja kwa msimu wa 2025/26.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.