Wapinzani wa Yanga SC Silver Strikers wameanza kiburi mapema, watua wakicheza

WAPINZANI wa Yanga SC, Silver Strikers wameanza kiburi mapema kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga SC, Oktoba 25,2025.

Yanga SC wanakibarua cha kusaka angalau ushindi wa mabao 2-0 ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Faida ya bao 1-0 walilopata ugenini limewapa kiburi ambapo waliwasili usiku wa Oktoba 23 huku wakicheza muziki kwa furaha na kubainisha kuwa mchezo utakuwa rahisi.

Mmoja wa wachezaji wa Silver Strikers aliweka wazi kuwa wanaamini watashinda mchezo wao dhidi ya Yanga SC kwa kuwa wao ni timu kubwa.

“Tunaamini kwamba tutapata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya wapinzani wetu, hatuna kitu cha kuhofia kwa kuwa hata sisi ni timu kubwa, baada ya mchezo tutaongea,” alisema mchezaji huyo.

Mchezo wa kesho Oktoba 25 2025 hakuna kiingilio na mageti yatafunguliwa saa nne asubuhi hivyo mashabiki wameombwa kujitokeza kwa wingi kuelekea katika mchezo huo muhimu.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.