Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Patrick Mabed kuwa Kocha msaidizi wa timu ya Yanga akiungana na kocha mkuu Romain Folz pamoja na msaidizi wake Mano Rodriguez
Mabedi amewahi kuwa Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Malawi kuanzia 2023 hadi 2025, lakini pia Mabedi aliwahi kuwa Mchezaji wa soka akipita kwenye vilabu kama Moroka Swallows ya (2006-2008), Kaizer Chief (1998-2006) zote za Afrika Kusini na Bata Bulleta ya Malawi (1989-1999).