JKT Queens ni washindi wa Ngao ya Jamii Wanawake 2025 wakiitwaa mbele ya Simba Queens katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Oktoba 12 2025.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Queens 2-1 Simba Queens ambapo dakika 45 za mwanzo mapema JKT Queens walipata goli la kuongoza.
Watupiaji ni Winfrida Gerald dakika ya 12 na Asha Omary alijifunga dakika ya 17. Goli pekee la kufuta machozi kwa Simba Queens lilifungwa dakika ya 90+5 na Zawadi Usanase dakika ya 90+5.
Mwaka 2024 JKT Queens walitwaa taji hilo kwa ushindi mbele ya Yanga Princess katika hatua ya fainali mwaka 2025 wametwaa taji hilo mbele ya Simba Queens.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.