Simba SC yatambia magoli mengi, kampeni inashika kasi

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa wachezaji wa timu hiyo wataongeza kasi kwenye eneo la kufunga magoli kutokana na falsafa mpya ya mwalimu.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa mwalimu mpya Dimitar Pantev anapenda kuona timu inashambulia kwa kasi jambo litakalokuwa ni furaha kwa Wanasimba.

Kwa sasa Ahmed anaongoza kampeni ya kataa jezi feki inayokwenda mkoa kwa mkoa walianzia Pwani kwa kupita Bagamoyo, Msata , Mkata kisha wakaingia mkoa wa Tanga lengo kuhakikisha mashabiki wananunua jezi Orijino kuongeza mapato kwa Simba SC na faida kwa mzabuni ambaye ni Jayrutty.

Kuhusu mwalimu mpya Ahmed amebainisha kuwa baada ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania kuna mengi yameanza kubadilika katika utendaji jambo ambalo litakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ushindani.

“Kwa namna ambavyo mwalimu wetu Pantev anapenda kushambulia kutakuwa na magoli mengi ambayo yatafungwa kwenye mechi zijazo. Alipotua kuna mengi yameanza kubadilika kiutendaji hivyo mashabiki wanapaswa kuwa na subira.

“Kikubwa ni ushirikiano kwa kuwa mwalimu anatambua yupo katika timu kubwa na ina wachezaji wenye ubora. Tupo tayari kwa ushindani na tutafanya vizuri.”

Miongoni mwa washambuliaji waliopo katika kikosi cha Simba SC ni Seleman Mwalimu, Steven Mukwala huku kwenye upande wa viungo washambuliaji kiongozi ni Jean Ahoua anayevaa jezi namba 10 mgongoni.

Oktoba 4 2025 Meneja Mkuu Dimitar Pentev alitua Bongo akiwa na msaidizi wake, Boyko Kamenov kwa ajili ya kuanza kuifundisha timu hiyo wakichukua mikoba ya Fadlu Davids ambaye ameajiriwa na Raja Casablanca.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.