Yanga na Romuald Rakotondrabe – Karibu Kila Kitu Kimekamilika

Taarifa kutoka Jangwani zinasema kuwa kwa sasa kwa kiwango cha 90%, Yanga SC na kocha Romuald Rakotondrabe wamekubaliana kila kitu; kilichobaki ni kocha kusaini mkataba rasmi na kutangazwa rasmi na klabu.

Yanga wameweka mezani mkataba wa miaka miwili, huku Romuald akionesha hamu kubwa ya kujiunga na kikosi cha mabingwa hao.

Kocha Rakotondrabe ni mtunzi wa mafanikio makubwa: amefanikisha Madagascar 🇲🇬 kufika fainali za CHAN, na timu yake ipo nafasi ya pili kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, nyuma ya Ghana kwa alama moja tu.