Mchezaji bora Septemba ni Diarra wa Yanga SC

Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga SC amekaa langoni katika mechi mbili ambazo ni dakika 180 amechaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya mwezi Septemba.

Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180 Diarra ameokoa hatari moja pekee ilikuwa katika mchezo dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine dakika ya 89 pigo la Vitalis Mayanga.

Katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC wapinzani hawakupiga shuti ambalo lililenga lango likamshughulisha kipa bora ndani ya Septemba msimu wa 2025/26.

Matokeo ya mechi ambazo Diarra alikaa langoni ilikuwa namna hii: Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC, Uwanja wa Mkapa

Mbeya City 0-0 Yanga SC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kipa huyo namba moja wa Yanga SC alikuwa anashindana na Anthony Trabi wa Singida Black Stars na Mohamed Bakari wa JKT Tanzania ambao aliingia nao katika hatua ya fainali.

Yanga SC kwenye msako wa pointi sita ilikomba nne, ikiangusha pointi mbili mchezo dhidi ya Mbeya City ugenini.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.