SIMBA SC imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Septemba 25 2025 wakikomba pointi tatu kwenye mchezo wa ufunguzi.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Rushine dakika ya 5 kwa pigo la kichwa akimalizia pigo la kona ya Jean Ahoua, Jean Ahoua dakika ya 36 kwa pasi ya Yusuph Kagoma na kamba ya tatu Jonathan Sowah dakika ya 57 kwa pasi ya Ellie Mpanzu.
Jean Ahoua ambaye amehusika katika mabao mawili kwenye mchezo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 kukamilika.
Katika mchezo wa kwanza wa Simba SC, safu ya ushambuliaji chini ya Sowah ilikwama kuonesha ubora wake ndani ya dakika 45 za mwanzo kutokana na kukosa umakini katika kumalizia nafasi ambazo zilikuwa zinatengenezwa na Jean Ahoua.
Sowah alikosa nafasi zaidi ya mbili kufanya majaribio katika kufunga huku kiungo Kibu Dennis akicheza katika kiwango ambacho hakikuwa bora ndani ya dakika 45 ambazo alicheza.
Beki Rushine katika mchezo wake wa kwanza wa ligi amekuwa miongoni mwa wachezaji wenye utulivu mkubwa akishirikiana na wachezaji wengine kwenye kuunda safu ya ulinzi makini akiwa na Shomari Kapombe, Moussa Camara ambaye ni mlinda mlango, Chamou.
Mchezo ujao kwa Simba SC ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, Uwanja wa Mkapa Septemba 28 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.