YANGA SC YAISOMA SIMBA SC KWA VIDEO KAZI IPO

DICKSON Job beki wa Yanga SC amefichua kwamba wachezaji wageni wamepewa video za wapinzani wao Simba SC ili watambue namna ya kukabiliana nao.

Miongoni mwa wachezaji wageni ndani ya kikosi cha Yanga SC ni Celestin Ecua ambaye kwenye mchezo wa Yanga Day dhidi ya Bandari alifunga bao akitumia pasi ya mshambuliaji Prince Dube.

Ecua anapewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa leo kutokana na kasi yake kwenye eneo la ushambuliaji.Yupo Mohamed Doumbia ambaye huyu amepewa jina la AI kutokana na kasi yake akiwa ndani ya uwanja.

Haya yote ni maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi wa Ngao ya Jamii, Yanga SC vs Simba SC unaotarajiwa kuchezwa leo Septemba 16 2025, Uwanja wa Mkapa.

Job amesema: “Kuna wachezaji ambao ni wageni kwenye timu hilo lipo wazi ila kuna video za mechi zetu zilizopita, benchi la ufundi linafanyia kazi malengo ni kuona tunapata matokeo mazuri.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa ni timu kubwa na huu ni mchezo wetu wa kwanza ambao una taji hivyo ni muhimu kufanya kazi kubwa kupata matokeo.Mashabiki tunaomba wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kutushangilia.”

Msimu wa 2024/25 Yanga SC ilitwaa taji la Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.