CHAMA AIPA UBINGWA SINGIDA BLACK STARS ATAJA SIRI

Kiungo mpya wa Klabu ya Singida Black Stars, Clatous Chama ameipa ubingwa wa kwanza timu hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa fainali Kagame Cup 2025.

Singida Black Stars ilitinga hatua ya fainali kwa kuifungashia virago KMC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Jumamosi ya Septemba 13 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 2-0 KMC, mabao yaifungwa na Chama aliyetupia bao moja na bao jingine lilifungwa na Ande Kofi.

Kwenye mchezo wa fainali Septemba 15 2025 ushindani ulikuwa ni mkubwa. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex, Septemba 15 ulisoma Al Hilal 1-2 Singida Black Stars. Al Hilal bao lao lilifungwa na Taha Abdelrazing dakika ya 31.

Chama ambaye alichaguliwa kuwa mfungaji bora alifunga mabao mawili dakika ya 20 na 57. Kiungo huyo ambaye aliwahi kucheza Simba SC na Yanga SC amebainisha kuwa siri ni nidhamu na kujituma.

“Nimefurahi kuona kwamba tumetwaa ubingwa hili ni jambo jema na kila mmoja amefurahi kwa kuwa tumekuwa tukifanya kazi kwa kushirikiana. Kikubwa ni nidhamu na kujituma kila wakati.”

Singida Black Stars ina wachezaji wenye uzoefu kuelekea msimu wa 2025/26 miongoni mwao ni kiungo mkabaji Khalid Aucho raia wa Uganda ipo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye aliwahi kuifundisha Yanga SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.