MASHABIKI WAJAA KWA WINGI MKAPA KUSHUHUDIA SIMBA DAY

Mashabiki wa Simba SC wamejitokeza kwa wingi muda huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kushuhudia tukio kubwa na la kipekee la Simba Day.

Hii ni siku maalum ambayo hutumika kuzindua kikosi kipya cha Simba kwa msimu mpya, kuwatambulisha wachezaji wapya, pamoja na burudani mbalimbali zinazochanganya muziki, michezo ya jukwaani na shamrashamra za mashabiki.

Uwanja tayari umejaa rangi nyekundu na kelele za vifijo, nyimbo na vuvuzela, huku mashabiki wakionekana na jezi mpya za klabu, bendera na mabango ya kuashiria mapenzi yao makubwa kwa wekundu wa Msimbazi.