HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA NBC 2025/26 MECHI ZA DABI

RATIBA ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 kwa sasa ipo wazi. Ni Septemba 17 2025 kivumbi kinarejea na mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz.

Hii hapa ratiba ya mechi za Dabi ndani ya ligi kwa msimu wa 2025/26 namna hii:-

 Watani wa jadi Yanga SC na Simba SC kuna dakika 180 ndani ya ligi wakiwa na Dabi ya Kariakoo. Mchezo wa raundi ya kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 13, 2025. Yanga SC atakuwa mwenyeji Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa pili wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa April 04, 2026. Mzunguko wa pili ni Simba SC atakuwa nyumbani. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Dar Dabi

Azam FC vs Yanga SC, mchezo wa kwanza ratiba yake itapangwa. Ni Azam FC watakuwa nyumbani na mchezo utachezwa Uwanja wa Azam Complex. Mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei 14 2026, Uwanja wa Mkapa muda utapangwa.

Mzizima Dabi

Hii huwakutanisha Simba SC vs Azam FC. Novemba 2 2025 mchezo wa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kuchezwa. Muda wa mchezo utapangwa ambapo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, Simba SC itakuwa nyumbani.

Mzunguko wa pili muda na tarehe utapangwa. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex. Wababe hawa watakutana kukamilisha ngwe ya pili.

Mbeya Dabi

Kuna timu mbili zenye ushindani mkubwa kutoka Nyanda za Juu Kusini, Mbeya. Ni Tanzania Prisons na Mbeya City. Oktoba 21 2025 itakuwa ni Mbeya City vs Tanzania Prisons na Machi 18 2026 itakuwa Tanzania Prisons vs Mbeya City, zote zitachezwa Uwanja wa Sokoine.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.