Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameikabidhi timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kiasi cha Milioni 200 za Kitanzania, wakati timu hiyo ikijiandaa kumenyana na Morocco katika mchezo wa robo fainali, utakaofanyika Agosti 22, 2025.
Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kiasi hicho cha fedha ni kama zawadi na hamasa kwa wachezaji hao wanapojiandaa na mchezo muhimu dhidi ya Morocco.