LADACK CHASAMBI KUONDOKA SIMBA SC

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi msimamo wake juu ya kiungo wake mshambuliaji, Ladack Chasambi kuwa hayupo katika mipango yake ya msimu ujao.

Kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akaondoka ndani ya kikosi cha Simba SC kwa msimu ujao ambapo inalezwa kuwa pengine anaweza kwenda KMC ama Namungo FC kwa mkopo.

Benchi la ufundi la Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni yeye ambaye amepewa jukumu la kufanya usajili kuelekea msimu mpya wa 2025/26 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo anapaswa kuondoka kabla ya dirisha alijafungwa kama akipata ofa nzuri kwingine kwa ajili ya changamoto mpya.