AZAM FC YAMALIZA KAMBI KARATU KWA KUTEMBELEA NGORONGORO

Leo Alhamisi, kikosi cha Azam FC kikiwa Karatu, mkoani Arusha, kimehitimisha kambi yake ya wiki mbili ya maandalizi ya msimu mpya kwa mtindo wa kipekee – kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro.

Ziara hiyo imekuwa sehemu ya kujivinjari na kuendeleza utalii wa ndani, ikiwapa wachezaji na benchi la ufundi nafasi ya kufurahia mandhari ya asili na urithi wa kipekee wa Tanzania baada ya mazoezi ya nguvu.

Wakiwa na tabasamu na shangwe, kikosi kimejionea moja ya maajabu ya dunia, kikipumzisha akili na miili huku kikijipanga kwa changamoto za msimu ujao.