YANGA YATOA UFAFANUZI KUHUSU MCHANGO WA CCM WA SHILINGI MILIONI 100

Uongozi wa Yanga SC umetoa ufafanuzi kuwa mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa CCM tarehe 12 Agosti 2025, ulitolewa na GSM Foundation inayosimamiwa na mdhamini wa klabu, Ghalib Said Mohammed, na haukutoka kwenye hela za wanachama au mfuko wa klabu.

Yanga pia imesema radhi kwa wanachama na mashabiki kwa sintofahamu iliyotokea kutokana na taarifa hiyo.