KENYA YAICHAPA MOROCCO, YATINGA ROBO FAINALI CHAN 2024

TIMU ya Taifa ya Kenya maarufu kwa jina la Harambee Stars imenadika rekodi yake kwa kutinga robo fainali CHAN 2024 kwa ushindi mbele ya wapinzani wao Morocco.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ilikuwa Kenya 1-0 Morocco. Ni Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Agosti 10 2025 pointi tatu zilibaki Kenya baada ya dakika 90.

Shujaa Mkenya ni Ryan Ogam aliyepachika goli la ushindi dakika 42 ya mchezo. Goli hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Licha ya Kenya kuwa pungufu kwa kuwa mchezaji mmoja alionyeshwa kadi nyekundu walikomaa mpaka mwisho.

Pointi hizo tatu zinawapa uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali. Kwenye Kundi A, Kenya wanaongoza Kundi. Pointi zao kibindoni ni pointi 7.

Huu hapa msimamo kwa Kundi A

Kenya inaongoza Kundi baada ya mechi 3 imekusanya jumla ya alama 7. Angola ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 4 kibindoni. Congo Dr ipo nafasi ya tatu ina pointi tatu.

Nafasi ya nne ni Morocco ikiwa na pointi tatu ilizokusanya. Ni mechi mbili imecheza ambazo ni dakika 180. Zambia inaburuza mkia baada ya mechi mbili haijakusanya pointi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.