DILI la kiungo wa Azam FC Feisal Salum kuibukia ndani ya kikosi cha Simba SC ni gumu kutokana na mkataba wake uliobaki na gharama za uhamisho ambazo zipo.
Ilikuwa inaelezwa kuwa Feisal anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC ilianza hivyo tangu dirisha dogo la msimu wa 2024/25.
Ipo wazi kwamba miongoni mwa viungo wazawa wenye uwezo mkubwa uwanjani, jina la Fei halikosekana kwa kuwa amekuwa kwenye mwendelezo wa ubora wake.
Msimu wa 2024/25 ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho ambazo alitoa 13 na alifunga mabao manne yote kwa mguu wa kulia.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna ugumu kwa kiungo huyo kuondoka Azam FC na kuibukia Simba SC hivyo Simba SC ina kazi kutafuta namba sita mwingine ambaye hatakuwa Fei Toto.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.