KHADIM ATAJWA KUIBUKIA SIMBA SC NI BEKI WA MPIRA

WAKATI beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye amedumu Msimbazi kwa miaka 11 akitajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga SC, inaelezwa kuwa kuna beki wa kazi anakuja kumalizana na Simba SC.

Chini ya Fadlu Davids, msimu wa 2024/25, Zimbwe Jr alicheza mechi 27 za ligi na alifunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo Simba SC iligawana pointi mojamoja na Coastal Union kwa ubao kusoma Simba SC 2-2 Coastal Union.

Taarifa zinaeleza kuwa Khadim Diaw  ambaye ni beki wa kushoto huenda akasaini dili ndani ya kikosi cha Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Diaw anaitumikia Al Hilal ni raia wa Mauritania hivyo anakuja Bongo ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.