KUELEKEA msimu mpya wa 2025/26, Simba SC wamebainisha kuwa watafanya usajili mkubwa kupata timu imara ya ushindani kitaifa na kimataifa.
Ipo wazi kuwa Aishi Manula ambaye ni kipa huyu atakuwa ndani ya Azam FC, Omary Omary amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha, Kelvin Kijili atakuwa ndani ya Singida Black Stars ni baadhi ya wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC msimu ujao.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wanakuja na kishindo. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Simba SC ilipishana na mataji yote iliyokuwa ikisaka.
Taji la Ngao ya Jamii ni Yanga SC walitwaa, taji la CRDB Federation Cup, Yanga SC walitwaa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC ni Yanga SC walitwaa huku lile la Kombe la Shirikisho Afrika ni RS Berkane ya Morocco walitwaa taji hilo.
Ally amesema wanatambua kwamba ulikuwa ni msimu wenye ushindani hivyo Wanasimba wasiishiwe nguvu, mipango inapangwa na usajili unafanyika mkubwa kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika kwa ajili ya kumalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe.”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.