WALLACE KARIA ASALIA PEKEE KINYANG’ANYIRO CHA URAIS TFF BAADA YA WAGOMBEA WATANO KUNG’OLEWA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, sasa amesalia kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 16, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, wagombea wengine waliokuwa wamejitokeza kuwania nafasi hiyo wameshindwa kutimiza sifa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF.