MUSONDA NA IKANGALOMBO KUKUTANA NA THANK YOU YANGA SC

INAELEZWA kuwa nyota wawili wa Yanga SC hawatakuwa ndani ya kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa ligi ya NBC msimu wa 2024/25.

Ni Jonathan Ikangalombo ambaye kwa msimu wa 2024/25 alipata nafasi kucheza mechi sita akitoa pasi mbili za mabao na straika Mzambia Kennedy Musonda ambaye alipata nafasi kucheza mechi 14 za ligi na kufunga mabao matatu.

Jonathan Ikangalombo amedumu Jangwani kwa miezi sita tu, sababu kubwa ikiwa ni winga huyo kupafomu chini ya kiwango alichotarajiwa na mabosi zake kuonyesha, hivyo mabosi wa Yanga SC wameamua kumpa mkono wa kwa heri.

Kandarasi ya Musonda imegota mwisho hivyo Yanga SC wanaingia sokoni kumtafuta mshambuliaji mwingine atakayekuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Nyota Musonda kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC, Novemba 5 2023 wakati ubao unasoma Simba SC 1-5 Yanga SC alifunga bao moja kwenye mchezo huo msimu wa 2023/24.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.