Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ameonyesha kushangazwa na mauno ya Queen Fraison maarufu kama Bonge la Dada, kupitia video iliyosambaa mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Kamwe aliandika kwa utani:
“Bora mimi nilikuwa naangalia nywele…” 😂😂😂😂
Kauli hiyo imeibua vicheko na mijadala miongoni mwa mashabiki, huku wengine wakiongeza maneno yao ya utani na maoni mbalimbali juu ya video hiyo inayomwonyesha Queen Fraison akionesha ujasiri na mvuto wa kipekee.
Queen Fraison ameendelea kuwa gumzo mitandaoni kutokana na muonekano wake na ujasiri wake wa kujiamini, huku akiwavutia maelfu ya wafuasi.