YANGA SC KINATOKA CHUMA KINAINGIA CHUMA

RAIS wa Yanga SC, Hersi Said ameweka wazi kuwa kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kinatoka chuma kinaingia chuma.

Juni 29 2025, Yanga SC ilitwaa taji la CRDB Federation Cup kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Walirejea Dar, Juni 30 2025 na kufanya parade la kihistoria ambalo lilianzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuanzia saa 4:00 asubuhi liligota mwisho saa majira ya saa tatu usiku.

Vituo ambavyo Parade la Kihistoria la Yanga SC iliyotwaa makombe matano msimu wa 2024/25 ni AirPort Terminal 1, Tazara, Keko, Karume, Msimbazi kwa watani zao wa jadi Simba SC na Jangwani.

Jangwani kulikuwa na shughuli ya burudani miongoni mwa wasanii waliowapa burudani Wananchi ni Mbosso Khan anayetamba na wimbo wake wa Aviola na alitambulishwa kuwa Mwananchi rasmi

Kuna wachezaji ambao wanaondoka Yanga SC ikiwa ni Kennedy Musonda na Aziz Ki huyu tayari ameondoka ndani ya Yanga SC yupo kikosi cha Wydad Casablanca.

Injinia amesema: “Kuna wachezaji ambao wanaondoka ndani ya kikosi cha Yanga SC, lakini wale wanaoondoka tunajua kazi ambayo wamefanya na mchango wao tunauheshimu. Wale ambao wanakuja tutahakikisha wanakuwa bora zaidi ili kuendeleza ubora wetu.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.