MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA 2024/25: YANGA BINGWA, SIMBA WAFUATA

Msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2024/25 umemalizika kwa kishindo kwa mchezo wa Kariakoo Derby, ambapo Yanga waliwafunga Simba 2-0 katika uwanja wa Mkapa. Pacome Zouzoua alifunga bao la kwanza kupitia penalti, na Clement Mzize akahitimisha ushindi huo kwa bao la pili dakika za lala salama. Ushindi huo uliwapa Yanga taji lao la 31 la NBC Premier League, wakiwa na pointi 82, nne zaidi ya Simba waliomaliza nafasi ya pili. Kwa upande wa wabashiri, msimu huu umekua bora kwa wale watumiaji wa meridianbet kwani fursa za pesa zilikua njenje.

Msimu huu, vilabu 16 vilishiriki, kila moja ikicheza michezo 30 (15 nyumbani, 15 ugenini). Yanga, Simba, Azam, na Singida Black Stars ziliibuka kidedea zikimaliza katika nafasi nne za juu. Yanga na Simba zitawakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, huku Azam na Singida zikielekea Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Kwa upande wa kushuka daraja, Kagera Sugar na Ken Gold zimetolewa Ligi Kuu, na nafasi zao zikachukuliwa na Mtibwa Sugar na Mbeya City. Tanzania Prisons na Fountain Gate bado ziko kwenye hatari, zikingoja mechi za mtoano (play-off) dhidi ya Stand United na Geita Gold ili kuamua hatima yao.

NB: Jiunge na Meridianbet na ujionee ushindi rahisi kupitia michezo mbalimbali ya kasino ya mtandaoni. Pia unaweza kuongeza kipato chako kwa kubashiri mechi zenye ODDS KUBWA. Piga *149*10# au tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz

Jean Ahoua wa Simba aliibuka mfungaji bora wa msimu kwa mabao 16, akifuatiwa na Clement Mzize wa Yanga (14). Na msimu huu ukishuhudia hat-trick za Prince Dube (dhidi ya Mashujaa), Ahoua (dhidi ya Pamba Jiji), Mukwala (dhidi ya Coastal Union), na Stéphane Aziz Ki (dhidi ya KMC). Sowah, usajili mpya wa dirisha dogo kwa Singida BS, akionyesha ubora wa hali ya juu kwa kufunga mabao 12 katika michezo 12 pekee.

Mousa Camara, kipa wa Simba, aliongoza mbio za kipa bora kwa kutokuruhusu bao lolote kwa jumla ya mechi 19, akifika rekodi ya Aishi Manula ya 2017/18, lakini akashindwa kuivunja baada ya kufungwa mara mbili na Yanga katika mechi ya mwisho.

Msimu huu ulishuhudia mabadiliko makubwa, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa waamuzi wa kigeni, ambao ulizua mijadala. Migomo ya vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kuhusu uamuzi wa bodi ya ligi ilisababisha mabadiliko ya uongozi ndani ya taasisi hiyo.

Takwimu za Msimu:

Mashambulizi: Yanga waliongoza kwa mabao 83, Simba 69, huku Pamba Jiji, Kagera Sugar, na Ken Gold zikiwa chini kwa kufunga mabao 22 kila moja.

Ulinzi: Yanga waliruhusu mabao 10 tu, Simba 13, na Azam 19. Ken Gold (62) na Fountain Gate (58) wakiwa na safu dhaifu zaidi za ulinzi.

Bila kusahau michezo yote ya ligi ilikua ikipatikana kwa ubashiri kupitia Meridianbet huku ikiwa na odds kubwa. Bado hujachelewa kwani michezo mingi bado ipo. Jisajili sasa na Meridianbet uanze safari yako ya kkutengeneza pesa kupitia ubashiri.