Yanga SC msimu wa 2024/25 wamevunja rekodi ya mabao yakufunga katika mechi za Ligi Kuu Bara ambayo waliiandika msimu wa 2023/24.
Yanga SC ilifunga mabao 71 baada ya mechi 30 na ilitwaa ubingwa wa ligi hivyo ni mabingwa watetezi.
Msimu wa 2024/25 baada ya mechi 28, Yanga SC imefunga jumla ya mabao 76 ongezeko la mabao matano ndani ya ligi.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 tuzo ya ufungaji bora ilichukuliwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Aziz Ki ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca.
Aziz alifunga jumla ya mabao 21 na alitoa pasi 8 za mabao ambazo zilimfanya ahusike kwenye mabao 29 yaliyofungwa na timu hiyo msimu uliopita na jina lake lilikuwa kwenye orodha ya wachezaji bora.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.