MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wametua Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.
Mchezo huo ni wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine kwa wababe hao kutafuta pointi tatu muhimu.
Yanga SC imebakiza mechi tatu, baada ya kumalizana na Prisons itakuwa na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kisha kete ya mwisho kwenye ligi ni dhidi ya Simba SC, Juni 25.