NGOMA ni nzito kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum kusepa ndani ya Azam FC kupata changamoto sehemu nyingine mpya kutokana na mabosi wa timu hiyo kuongeza dau upande wa mshahara.
Fei amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC ambazo zinapigana vikumbo kusaka saini yake.
Ipo wazi kwamba Fei ni namba moja kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika akiwa ametengeneza jumla ya pasi 13 ndani ya kikosi cha Azam FC msimu wa 2024/25.
Azam FC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tatu kwa sasa ipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya 29 utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Juni 18 2025.
Mchezo huo utakuwa dhidi ya Tabora United kwenye msako wa pointi tatu muhimu katika kukamilisha mzunguko wa pili.
Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo ambaye mkataba wake umesalia mwaka mmoja mabosi wa Azam FC wapo kwenye mazungumzo naye ili aongeze mkataba mwingine hivyo ngoma itakuwa nzito kwa timu nyingine kupata saini yake.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.