KIPA SIMBA SC ATAJWA AZAM FC

KIPA wa Simba SC, Aishi Manula inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji saini yake.

Ipo wazi kwamba Manula kwa msimu wa 2024/25 hajawa chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids.

Katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara hajaanza langoni mchezo hata mmoja na kwenye anga la kimataifa pia jina lake lilikuwa linaondolewa kwenye siku za safari.

Kwenye mechi zote za fainali ugenini na Tanzania, dhidi ya RS Berkane ni Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC alianza na benchi alikuwa Ally Salim.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Azam FC wanahitaji saini ya kipa huyo ambaye ni miongoni mwa wazawa wenye uwezo mkubwa awapo langoni.

Ikumbukwe kwamba wakati wa dirisha dogo Azam FC walituma maombi kwa Simba SC kuhitaji huduma ya Manula ila mabosi wa Simba SC wakabainisha kuwa bado wanahitaji huduma yake.

Julai 2022, Air Manula aliongeza mkataba na Simba SC ambao unatarajiwa kugota mwisho msimu wa 2024/25 ukifika tamati.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.