WABABE wawili ndani ya ardhi ya Tanzania kwenye eneo la mpira wa miguu ndani ya ligi ya vijana huko kwao mambo ni magumu kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayaoata ndani ya uwanja.
Ni Yanga SC na Simba SC katika NBC Youth League 2024/25 mambo ni magumu kwao kutokana na mwendo ambao wapo nao katika makundi tofauti waliyopo kila mmoja kwa wakati wake.
Katika nane bora, Yanga SC Youth ipo kundi B ambalo kinara ni Kagera Sugar mwenye jumla ya pointi 4 baada ya mechi mbili ndani ya dakika 180.
Ushindi ni kwenye mchezo mmoja na sare mchezo mmoja huku safu ya ushambuliaji ikitupia mabao matatu na imeruhusu kifungwa bao moja.
Yanga SC Youth ni nafasi ya nne baada ya mechi mbili zote imepoteza ilianza Yanga SC 1-2 Tanzania Prisons kisha ikapoteza kwa kufungwa mabao 32 dhidi ya Fountain Gate iliyo nafasi ya pili.
Simba SC Youth kwenye kundi A nafasi ya tatu na pointi mbili baada ya kucheza mechi tatu imepoteza moja na kuambulia sare mbili kwenye mechi ambazo ilishuka uwanjani.
Kwenye kundi A vinara ni Azam FC wenye pointi 7, nafasi ya pili ni KenGold yenye pointi 6, nafasi ya tatu ni Simba SC yenye pointi 2 na nafasi ya nne ni Dodoma Jiji yenye pointi moja.
Kwenye kundi B vinara ni Kagera Sugar weye pointi nne, Fountain Gate wenye pointi nne nafasi ya pili, nafasi ya tatu ni Tanzania Prisons wenye pointi tatu na Yanga SC nafasi ya nne haijavuna pointi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.